Jumatano 28 Oktoba 2026 - 15:40
Wananchi wa Tunisia Wakusanyika Kuitetea Palestina; Hii ni Awamu ya 143

Hawza/ Katika hali ya kuendelea mashambulizi ya uchokozi na sera ya kimfumo ya utawala wa Kizayuni ya kuwasababishia njaa wakazi wa Ukanda wa Ghaza, mitaa ya Tunisia imeendelea kusisitiza kushikamana na misingi ya suala kuu la Umma wa Kiislamu kwa kuandaa mkusanyiko wake wa mara kwa mara wa 143 mbele ya Ukumbi wa Maonesho wa Manispaa ya Tunisia.

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, chini ya kaulimbiu mashuhuri isemayo, “Ghaza Inakabiliwa Tena na Njaa… Vunjeni Mzingiro… Okoeni Maisha,” mkusanyiko wa mara kwa mara wa 143 ulifanyika mbele ya Ukumbi wa Maonesho wa Manispaa katika mji mkuu wa Tunisia, kutokana na wito wa Jumuiya ya Wafuasi wa Palestina na wanachama wa Muungano wa Tunisia wa Kusaidia Haki za Palestina.

Maana ya Mwendelezo wa Harakati Katika Mapambano ya Kuimarisha Uelewa

Mkusanyiko huu una umuhimu mkubwa kwa sababu unaonesha hali ya kukataa kusahau na kukataa kuzoea mandhari ya uharibifu.

Kwa zaidi ya mikusanyiko 103 ya mara kwa mara, mitaa ya Tunisia imethibitisha kwamba mapigo ya moyo wa mshikamano hayajadhoofika, na kwamba kutegemea kupita muda na kuchoka mataifa hakutakuwa na mwisho wala hatima nyingine isipokuwa kushindwa.

Tukio hili liliandaliwa kwa lengo la kuangazia janga la kibinadamu linalozidi kuwa baya huko Ghaza, hususan kivuli kibaya cha njaa ambacho wavamizi wanajaribu kukitumia kama silaha ya ziada ya kuwalazimisha raia kujisalimisha, huku kukiwa na ukimya wa kimataifa wenye kuaibisha.

Malengo na Vipengele vya Harakati Hii

Swa'diq Ammar, mwenyekiti wa Muungano wa Tunisia wa Kusaidia Haki za Palestina, alipokuwa akifafanua vipengele na malengo ya kimkakati ya harakati hii ya mapambano, alisisitiza kuwa: “Ujumbe wetu uko wazi: Ghaza inakabiliwa tena na sura mbaya zaidi ya adhabu ya pamoja na sera ya kimfumo ya wavamizi ya kuwasababishia njaa wakazi wake, katika mazingira ya njama za kushirikiana na ukimya wenye kuaibisha kutoka kwa jumuiya ya kimataifa. “Kufikia kwetu mkusanyiko wa 143 si idadi tu, bali ni ushahidi thabiti kwamba mitaa ya Tunisia haijawahi kuchoka wala kukata tamaa, na wala haitachoka wala kukata tamaa. Suala la Palestina linaendelea kuwa hai katika dhamiri zetu leo, kesho na kila wakati.

“Leo tumetaka kuifikisha sauti yetu kwa ulimwengu mzima, kwamba mzingiro uliowekwa dhidi ya ndugu zetu wapendwa katika Ukanda wa Ghaza ni uhalifu wa kivita ambao lazima uvunjwe mara moja kwa kutumia njia zote zinazowezekana.”

Akizungumzia mbinu za utekelezaji wa shughuli za muungano huo na umuhimu wa shinikizo la wananchi, aliongeza kusema: “Lengo letu kuu ni kuendeleza mshikamano na kuugeuza mshikamano huu wa kihisia na suala la Palestina kuwa shinikizo la wananchi lililo halisi, lenye nguvu na lenye kuleta athari.

“Tunafanya kazi katika nyanja mbalimbali, ambazo muhimu zaidi ni kuimarisha kampeni za wananchi za kususia bidhaa na kampuni zote zinazounga mkono utawala wa kinyakuzi, kufichua sauti zote za kujisalimisha na kuhalalisha uhusiano na Israel, pamoja na kuendeleza shinikizo la mara kwa mara kwa ajili ya kuunga mkono mipango ya kibinadamu na misafara inayolenga kuvunja mzingiro. “Tunaamini kwamba mataifa yaliyo hai yana uwezo wa kuleta mabadiliko na kulinda dira yake dhidi ya upotoshaji.”

Mwenyekiti wa muungano huo, katika hitimisho lake, akizungumzia matumaini ya adui kwamba muda utapita na jamii itachoka, alisisitiza kuendelea harakati hizi bila kusimama, akisema: “Umuhimu wa mikusanyiko hii unatokana na nafasi yake kama mapambano ya kuimarisha uelewa. Adui anategemea kupita muda na anatumaini kwamba mataifa ya Kiarabu yatachoka na kuisahau Ghaza. “Kwa sababu hiyo, uwepo wetu wa mara kwa mara mitaani na mbele ya Ukumbi wa Maonesho wa Manispaa ni tangazo la wazi la changamoto na uthibitisho wa kushikamana na ahadi yetu. “Tunawaambia kwamba hatutanyamaza, hatutaiacha Ghaza peke yake, wala hatutaachia hata shubiri moja ya ardhi ya manabii, mpaka ushindi wa jumla upatikane na sote tuswali katika viwanja vya Msikiti wa Al-Aqsa uliobarikiwa.”

Mkusanyiko wa 143 katika mji mkuu wa Tunisia ni mfano hai unaoonyesha uwezo wa jamii ya kiraia katika kudumisha nafasi ya Palestina katika kitovu cha mijadala na uangalizi wa umma.

Harakati hii imegeuza hasira ya wananchi kuwa nyenzo za shinikizo la vitendo, kama vile kususia bidhaa na kufichua sera za kuwasababishia watu njaa. Pia, inatoa ujumbe ulio wazi kwamba; mshikamano wa Tunisia na Ghaza ni mkakati wa muqawama unaoendelea ambao hautakoma mpaka mzingiro uondolewe na uhuru kamili upatikane.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha